Wakenya waadhimisha sikukuu ya Mazingira

Dismas Otuke
0 Min Read

Ijumaa, Oktoba 10 kila mwaka imetengwa kuwa sikukuu ya mazingira nchini Kenya.

Siku hii awali ilikuwa sikukuu ya Moi kabla ya kubadilishwa na kuwa siku ya mazingira mwaka uliopita.

Siku hii imetengwa mahususi kwa shughuli za utunzaji mazingira, ikiwemo upanzi wa miti katika juhudi za serikali za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kenya imelenga kupanda miti bilioni 15 kufikia mwaka 15 kupitia mpango wa “Jaza Miti.”

 

Share This Article