Wakenya kuwinda nishani kwenye fainali mbili leo Tokyo

Dismas Otuke
1 Min Read

Wanariadha wa humu nchini watalenga kujiongezea nishani zaidi katika siku ya tano ya mashindano ya Riadha Duninia mjini Tokyo Japan leo jioni.

Mshindi wa nishani ya shaba ya dunia mwaka 2023 Faith Cherotich atashiriki fainali ya mita 3000 kuruka viunzi na maji kuanzia saa tisa na dakika 57 alasiri, akilenga kutwaa dhahabu ambayo ilinyakuliwa na Wakenya kwa mara ya mwisho mwaka 2019.

Cherotich aliye na umri wa miaka 21 atashirikiana na Doris Lemngole kwenye fainali hiyo huku upinzani ukitarajiwa kutoka kwa Mkenya anayekimbilia Bahrain Winfred Yavi na bingwa wa Olimpiki mwaka 2020 Peruth Chemtai.

Baadaye saa kumi na dakika 20 bingwa wa Dunia mwaka 2019 Timothy Cheruiyot na bingwa wa zamani wa Dunia kwa chipukizi Raynold Cheruiyot watatimka fainali ya mita 1500.

Kenya ni ya pili kwenye msimamo wa medali baada ya siku nne za mashindano hayo ikiwa na medali 5 ,dhahabu 3 fedha 1 na shaba 1.

Marekani inaongoza kwa dhahabu 6 na shaba  2.

Share This Article