Wakazi wa Watamu waimarisha juhudi za kuwavutia watalii

Tom Mathinji
2 Min Read
Wakazi wa Watamu waimarisha juhudi za kuwavutia watalii.

Katika juhudi za kuboresha madhari ya utalii na kuvutia wageni haswa katika mji wa kitalii wa Watamu, vuguvugu la chama cha wamiliki wa maboti kiliandaa hafla ya kusafisha fukwe za Bahari hindi katika maeneo ya Watamu kama njia mojawapo ya kuhamazisha jamii umuhimu wa usafi katika kuboresha mazingira ya kuhifadhi sehemu za kitalii na kuvutia wageni.

Washika dau hao wana matumaini kakubwa ya ongezeko la idadi ya watalii mwaka huu wanapojiandaa kuanza msimu mpya.

Walizungumza wakati wa sherehe za kila mwaka za kusafisha ufuo kuashiria mwanzo wa msimu, zilizoandaliwa na wamiliki wa boti za Watamu na jamii ya watamu wanapania kuanza vyema huku wakipanga kuboresha watamu kama sehemu bora ya ufuo inayotoa bidhaa tofauti kama Safari blue excursion.

Hussein Ahmed Abdi ambaye ni mweka hazina wa jamii ya Watamu wamiliki na waendeshaji boti,  alisema wana matumaini ya kupata bahati nzuri wanapoanza msimu wa juu wa 2025 – 2026 kwa kusafisha mfumo wa ikolojia pamoja na jamii ya watamu na shule kama sehemu ya CSR yao ili kukuza bidhaa na pia kufanya maombi na chakula cha bure kwa jamii kama mbali na kubariki msimu.

Pia alipongeza ushirikiano wa KWS katika watamu kwa kukuza utalii endelevu ambapo mapato yatokanayo na mapato yanayokusanywa yanaenda pia katika kukuza miradi ya jamii katika kipindi cha miaka sita hivi leo kikundi hicho kina Ambulance ya kijamii kusaidia kukabiliana na dharura za matibabu, Makanisa na misikiti pia imenufaika na jenereta za bure zenye vipaumbele katika kusomesha watoto yatima wa watamu.

Hata hivyo alisema kuzinduliwa kwa maadhimisho haya ya kila mwaka ya jamii kabla ya msimu huu ni kielelezo tu cha kujenga uhamasishaji wa soko la marudio na ushirikiano wa jamii kufaidika na bidhaa hiyo.

TAGGED:
Share This Article