Wakazi wa kajiado wapokea hatimiliki za ardhi

Tom Mathinji
1 Min Read
Wakazi wa Kajiado wapokea hatimiliki za ardhi.

Wamiliki ardhi katika kaunti ya Kajiado wana sababu ya kutabasamu, baada ya kupokea hati za kumiliki ardhi kutoka kwa serikali ya kaunti hiyo.

Walionufaika katika  zoezi hilo lililoongozwa na Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku ni wamiliki ardhi kutoka maeneo ya Noonkopir, Isinya, Bulbul, Kajiado na Namanga.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Lenku alisema hatua hiyo inatimiza ahadi alizotoa kwa wakazi wa Kajiado, ikiwa ni pamoja na kutekeleza mipango ya usimamizi wa ardhi kwa ushirikiano na idara za ardhi, mipango na maendeleo ya mijini.

“Hatua hii ni ishara ya yale tunayoweza tekeleza iwapo tutafanyakazi pamoja,” alisema Lenku.

Wakazi wa Kajiado wapokea hatimiliki za ardhi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Ardhi Kabale Tache Arero, alisema hatimiliki 8000 zinashughulikiwa na zitatolewa kwenye awamu ifuatayo.

“Nawapongeza wamiliki ardhi wa mijini kaunti ya Kajiado kwa kuunga mkono mchakato kwa rasilimali zilizohitajika,” alisema Arero.

Serikali ya kaunti ya Kajiado imepunguza ada ya kupata hati za kumili ardhi kutoka shilingi 300,000 hadi shilingi 55,000, hatua ambayo imefanikisha wakazi hao kumiliki ardhi mijini.

Share This Article