Waititu mashakani kisiasa kufuatia uamuzi wa mahakama?

Dismas Otuke
1 Min Read

Uamuzi wa Jumanne iliyopita wa kumpata na hatia ya ufisadi wa shilingi milioni 588, Gavana wa zamani wa kaunti ya Kiambu, Ferdinand Waititu, huenda ukawa mwisho wa azma yake ya kisiasa.

Waititu aliyekuwa amerejea katika ulingo wa kisiasa akiashiria kujipanga kuwania kiti katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, sasa atafungiwa kugombea nafasi yoyote wala kupata uteuzi wowote wa ofisi ya umma.

Waititu pamoja na mkewe, Susan Wangari, na wakurugenzi wa kampuni ya Testimony Enterprises, Charles Chege na Beth Wangeci, walipatikana na hatia ya kesi za ufisadi.

Gavana huyo wa zamani alitimuliwa afisini miaka mitano iliyopita kwa tuhuma za ufisadi.

Katika siku za hivi karibuni, Waititu, almaarufu Baba Yao, amekuwa akiegemea mrengo wa kisiasa unaowaleta pampja kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, Eugene Wamalwa na Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua.

Viongozi hao wameahidi kutangaza jina la muungano wao mpya wa kisiasa katika hatua itakayoashiria rasmi kuzikwa kwa muungano wa Azimio katika kaburi la sahau.

Share This Article