Waislamu watarajiwa kuanza mfungo wa Ramadhani

Dismas Otuke
1 Min Read

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa Waislamu wote ulimwenguni unatarajiwa kuanza leo Ijumaa hadi Machi 30.

Waislamu hufunga kula chakula wakiomba katika mwezi wa Ramadhani kuanzia macheo hadi machweo katika mwezi wa tisa wa Hijri na hufanyika kila mwaka.

Mfungo huanza rasmi punde baada ya kuandama kwa mwezi na hudumu kwa kipindi cha mwezi mzima.

Wakati wa mfungo, Waislamu hujinyima kula na kunywa na starehe zote, huku wakiomba ili kuafikia utakaso wa mungu maarufu kama taqwa.

Hata hivyo, endapo mwezi hautaandama leo, mwezi wa mfungo utaanza tarehe 2 mwezi Machi.

Rais William Ruto amewatakia Waislamu wote nchini Ramadhani njema.

Share This Article