Zaidi ya Waislamu bilioni 1.8 kote duniani, leo Jumamosi wameanza mwezi mtukufu wa Ramadhan baada ya kuonekana kwa mwezi nchini Saudi Arabia.
Mwezi wa Ramadhan huanza punde tu baada ya kuonekana kwa mwezi, ambapo waumini wa Kiislamu hufunga kula au kunywa kwa muda wa mwezi mzima.
Mwezi huo huadhimishwa kila mwaka, katika mwezi wa tisa wa Hijri na kuwapa Waislamu muda wa kutafakari kuhusu maswala ya kiroho.
Katika maombi ya Ijumaa Jijini Nairobi, viongozi katika misikiti mbali mbali walitoa wito kwa waumini wa Kiislamu kuwasaidia wasiojiweza katika jamii.
Mwezi huo mtukufu, unatarajiwa kukamilika Machi 30, 2025,huku sherehe za Eid al Fitr zikitarajiwa kuanza wakati huo kukiwa na uwezekano utofauti wa siku kadhaa.