Wahadhiri wa vyuo vikuu waanzisha mgomo

Marion Bosire
1 Min Read
Constatine Wasonga, Katibu mkuu UASU

Wahadhiri wa vyuo vikuu humu nchini wameanzisha mgomo wao hatua ambayo itaathiri pakubwa shughuli za masomo katika vyuo vikuu vya umma nchini.

Chama cha wahadhiri hao UASU kimetangaza kwamba mgomo huo utaendelea hadi pale ambapo serikali itatimiza matakwa yao kama yaliyo kwenye makubaliano ya pamoja ya mwaka 2012 hadi 2025.

Katibu mkuu wa UASU Constantine Wasonga, anaitaka serikali itekeleze yaliyomo kwenye mapatano na mpango wa kurejea kazini ulio na mengi mazuri kwa maslahi yao.

Wahadhiri hao wameapa kutorejea kazini hadi walipwe pesa wanazodai huku wakishtumu manaibu chansela wa vyuo vyao kwa kuwa kizingiti kwa mipango yao ya kutafuta malipo bora.

Wasonga amesisitiza hakuna mhadhiri ataonekana kwenye kumbi za masomo kutoa huduma kwa wanafunzi hadi matakwa yao yatimizwe.

Mwisho wa mwezi Septemba mwaka huu wa 2024, wahadhiri walisitisha mgomo baada ya kuafikia makubaliano na serikali kwamba wangeongezwa mshahara kwa asilimia 10.

Walikuwa wametoa ilani ya siku saba ya kugoma iliyokamilika jana usiku wa manane.

Share This Article