Wagombea kadhaa wa ODM wakabidhiwa vyeti vya uteuzi

Martin Mwanje
1 Min Read
Aliyekuwa mbunge wa Magarini Harrison Kombe ni miongoni mwa waliokabidhiwa vyeti vya uteuzi

Jumla ya wagombea 7 wamekabidhiwa vyeti vya uteuzi vya bwerere na chama cha ODM kuelekea chaguzi ndogo zilizopangwa kufanyika Novemba 27. 

Katika eneo bunge la Magarini, Harrison Kombe amekabidhiwa tiketi ya kutetea tena kiti chake alichopoteza baada ya mahakama kufutilia mbali kuchaguliwa kwake mwaka jana.

Katika ngazi ya wadi, Salimu Mohamed atapeperusha tiketi ya chama cha ODM katika wadi ya Chewani, kaunti ya Tana River.

Huko Kakamega, Thomas Eshuya Oyolo atagombea uwakilishi wadi kwa tiketi ya chama cha chungwa katik wadi ya Kisa Mashariki huku Daniel Naikuni akisaka wadhifa huo katika wadi ya Purko, kaunti ya Kajiado.

Wengine waliokabidhiwa vyeti vya uteuzi na ODM kugombea uwakilishi wadi ni Letoluai Loisia (Angata Nanyokie), Feisal Gedi (Fafi) na Mohammed Yussuf (Naanam).

 

 

Share This Article