Wafuasi wa upinzani nchini Tanzania, wakiongozwa na wale wa chama cha Chadema, wamejuriwa leo katika makabiliano makali na polisi waliowazuia kufika mahakamani.
Wafuasi hao wakiongozwa na baadhi ya wanasiasa walitaka kufika mahakamani eneo la Kisutu viungani mwa Dares Salaam, kufuatilia kesi ya kiongozi wa Chadema Tundu Lissu, aliyeshitakiwa kwa kosa la uhaini na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Joto la kisiasa inazidi kupanda huku Tanzania, ikijiandaa kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu, ambapo Rais Samia, anawania kuhifadhi kiti chake kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM).