Wachezaji wa Nigeria wamaliza mgomo

Dismas Otuke
1 Min Read

Wachezaji wa timu ya taifa ya Nigeria wamemaliza mgomo na kurejea mazoezini mapema leo nchini Morocco kujiandaa kwa mechi ya nusu fainali dhidi ya Gabon kufuzu kwa Kombe la Dunia leo usiku.

Super Eagles itakabiliana na Gabon kaunzia saa moja mjini Rabat katika nusu fainali hiyo ya kwanza ya mchujo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Awali wachezaji wa Nigeria walisusia mazoezi kuanzia mapema wakidai malimbikizi ya marupurupu ya mechi za awali na pia marupurupu ya kufuzu kwa Kombe la AFCON.

Kulingana na Nahodha William Troost Ekong, shirikisho la soka la Nigeria, NFF, liliwapa wachezaji marupurupu ya siku ya Jumatano.

Mshindi wa nusu fainali hiyo atakutana na mshindi wa semi fainali ya pilikati ya Cameroon na DR Congo katika fainali ya Jumapili Novemba 16.

Share This Article