Wachezaji 9 watemwa kutoka kikosi cha Malkia Strikers

Kikosi cha mwisho kitatangazwa kabla ya timu hiyo kuelekea Vietnam baina ya Agosti 15 na 20 kwa mechi za kujipima nguvu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wachezaji tisa wamedondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Mpira wa wavu kwa wanawake, inayojiandaa kwa mashindano ya dunia nchini Thailand kati ya Agosti 22 na Septemba 7 mwaka huu.

Kikosi hicho ambacho kimekuwa mazoezini katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo kilipunguzwa kutoka wachezaji 29 hadi 20 na baadaye kitachujwa hadi kusalia 14 mapema mwezi ujao.

Wachezaji waliopigwa shoka ni pamoja na Valerie Chepkoech, Vivian Vugutsa, Peninah Wafula, Sharon Sandui, Valentine Jemutai, Miriam Musa, Deborah Sang, na Lydia Iswan.

Kikosi cha mwisho kitatangazwa kabla ya timu hiyo kuelekea Vietnam baina ya Agosti 15 na 20 kwa mechi za kujipima nguvu.

Kikosi cha awali

Maseta: Emmaulate Nekesa, Fridah Boke, Marclean Okoko

Washambulizi : Mercy Iminza, Malyne Terry, Loice Simiyu, Pamela Adhiambo,Daisy Leting, Veronica Adhiambo, Juliana Namutira, Sarah Namisi, Meldina Sande

Walinzi:Belinda Barasa, Elizabeth Sokoiyo, Gladys Ekaru, Lorine Chebet, Pauline Chemtai

Malibero: Celestine Nafula, Sharlene Maywa, Dolphine Misoki

Kenya imo kundi G katika mashindano ya dunia ya mwaka huu ya kati ya Agosti 22 na Septemba 2 pamoja na Ujerumani, Poland, na Vietnam.

Geoffrey Omondi ndiye kocha mkuu akisaidiwa na Esther Jepkosgei na David Muthui.

Share This Article