Wabunge wamekemea vikali matamshi ya Rais William Ruto kuwahusisha na kupokea hongo kwenye kamati zake ili kupitisha miswada.
Wabunge katika bunge la kitaifa wamemtaka Rais Ruto kuitwa bungeni kufafanua madai hayo huku Maseneta wakisitisha vikao vya kamati zake.
Aidha, wamesema matamshi na madai ya Rais Ruto yanapaka tope na kushusha hadhi ya bunge.
Awali katika bunge la Seneti lilitishia kuwang’atua Maspika wa Mabunge yote kwa kushindwa kutetea taasisi hizo.
Rais alisema alidai kuwa baadhi ya wanachama na wenyeviti wa kamati za bunge hupokea hongo ya hadi shilingi milioni 10 kupitisha miswada.