Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki EALA, wamemtaka mwenyeki wa Jumuiya ya EAC Rais William Ruto, kuitisha kikao cha Marais, kujadili ukosefu wa fedha ambao umelemaza shughuli za bunge hilo.
Kupitia kikao cha mtandaoni wakati wa kupitisha bajeti ya mwaka 2025 na 2026, wabunge hao wameapa kutolegeza kamba hadi kamati tekelezi ya bunge hilo itakapopokea pesa za kuendesha shughuli.
Shughuli nyingi za Bunge hilo zimekwama kutokana na uhaba wa pesa.