Leo ni siku ya pili tangu serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, itangaze kuzima mtandao wa X, kwa kile ilichokitaja kuwa uenezaji wa video na picha za ngono kwa raia wake kupitia mtandao huo.
Makundi ya kijamii nchini humo yamelaani vikali hatua hiyo inayokiuka sheria, tamaduni, na itikadi za raia wa Afrika Mashariki.
Yamkini mtandao huo wa X ulikuwa umebanwa ingawa hakukuwa umefungwa kabisa kwa majuma mawili yaliyopita wakati joto la kisiasa lilikuwa limepanda nchini humo.
Pia, mtandao wa Telegram, haupatikani nchini Tanzania kwa sasa.
Hata hivyo, kilichowakera raia zaidi ni hatua ya maafisa wa serikali kuendelea kutumia mtandao huo, huku wakiwazimia wananchi.
Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Jerry Silaa, alisema hatua hiyo ya kufunga kabisa mtandao wa X inalenga kulinda raia wake.