Waasi wa M23 waliua watu 140 Julai mashariki ya DRC

Yamkini mapigano yanaendelea mashariki ya Congo, licha ya mwafaka wa kusitisha mapigano kusainiwa kati ya M23 na serikali ya DRC.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na serikali ya Rwanda waliwauwa raia 140 mwezi jana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa mujibu wa ripoti ya watetezi wa haki za kibinadamu.

Hata hivyo, idadi hiyo ya waliouawa huenda ikapita 300, baada ya Umoja wa Mataifa pia kuripoti mauaji ya halaiki na kundi la M23 mwezi Julai.

Yamkini mapigano yanaendelea mashariki ya Congo, licha ya mwafaka wa kusitisha mapigano kusainiwa kati ya M23 na serikali ya DRC.

Share This Article