Raia 98 walioshiriki maandamano ya Oktoba 29 baada ya uchaguzi nchini Tanzania wamefunguliwa mashtaka ya uhaini leo Ijumaa.
Haya yanajiri huku upinzani ukidai kuwa zaidi ya watu 1,000, waliuawa wa kupigwa risasi na polisi katika miji mbalimbali wakati wa maandamano hayo yaliyozuka siku ya uchaguzi mkuu.
Mashtaka hiyo inasema kuwa watu hao walijaribu kuzuia uchaguzi mkuu kw ania ya kudhallisha serikai na kufanya uharbifu wa mali ya umma na ile ya kibinafsi.
Viongozi wa kidini hata hivyo wamemtaka Rais Samia Suluhu kuongoza maridhiao ya kitaifa wakihisi kuwa mashtaka hayo yataongeza uhasama .
Tume ya uchaguzi ilimtangaza Samia kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kuzoa asilimia 98 ya kura zilizopigwa.