Takriban waandamanaji 111 waliokamatwa katika maadhimisho ya 35 ya saba saba Jumatatu iliyopita, waliachiliwa huru jana kwa dhamana ya shilingi 50 kila mmoja na Mahakama ya kisheria ya Nanyuki.
Hakimu mkazi wa mahakama hiyo Emmaculate Deche, alisema hakukuwa na sababu tosha kutoka upande wa mashtaka za kuendelea kuwaweka rumande washukiwa hao, ambao wengine walitiwa mbaroni mkesha wa siku ya Saba Saba.
Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 29 mwezi huu.