Visa 19 vya wizi wa mtihani wa KCSE vimeripotiwa, asema Waziri Ogamba

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri Julius Ogamba akiwa mjini Machakos

Jumla ya visa 19 vya wizi wa mtihani unaoendelea wa kidato nne, KCSE vimeripotiwa nchini kufikia sasa. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu Julius Ogamba leo Ijumaa asubuhi wakati akifungua kontena ya karatasi za mtihani huo mjini Machakos.

Ogamba anasema visa vingi vimeripotiwa eneo la Nyanza, Bonde la Ufa na maeneo ya Mashariki huku serikali ikichukulia hatua vituo husika.

Ameongeza kuwa tayari vituo vitatu vya mtihani vimeanza kuchukuliwa hatua za kisheria na huenda vikapigwa marufuku.

Waziri akielezea kuwa tayari vituo vitatu vya mtihani vimenza kuchukuliwa hatua za kisheria na huenda zikapigwa marufuku.

Ripoti za wizi wa mtihani unaoendelea wa KCSE zimezagaa tangu kuanza kwa mtihani huo huku watu kadhaa, wakiwemo wasimamizi wa mtihani na walimu wakuu wakikamatwa.

Hali kadhalika, Waziri amekanusha madai madai ya kuongezwa kwa karo ya shule za sekondari mwakani kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Ripoti hizo zilidai kuwa karo hiyo itaongezwa hadi shilingi 53, 554 kwa mwaka kutoka shilingi 22, 244 za awali.

Share This Article