Kenya Pipeline ndio mabingwa wa Ligi Kuu ya Voliboli kwa wanawake msimu wa mwaka 2024/2025, baada ya kukabiliwa na upinzani mkali kabla ya kuwaangusha DCI seti 3-2 Jumamosi alasiri katika ukumbi wa Kasarani.
Pipeline walipoteza seti ya kwanza 21-25, kabla ya kunyakua seti ya pili 25-21 na kupoteza ya tatu 18-25.
KPC walisisimka na kutwaa seti mbili za mwisho , 25-21 na 15-11, na kuvishwa ubingwa.
Pipeline ambao ni mabingwa mara tano wa Afrika wamenyakua taji hiyo waliyoshinda kwa mara ya mwisho mwaka 2022.
Kenya Commercial Bank walimaliza katika nafasi ya tatu kufuatia ushindi wa seti 3-1 za (27-25, 25-14, 25-20, 25-14) dhidi ya Kenya Prisons .