Vipusa wa Kenya watoswa nje ya Voliboli ya Dunia

Malkia walipoteza seti ya kwanza kwa alama 17-25, ila wakajizatiti na kunyakua seti ya pili 25-15.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ya voliboli kwa wanawake, Malkia Strikers, ilitemwa nje ya mashindano ya Dunia baada ya kuambulia kichapo cha seti 3-1, dhidi ya Poland jana jioni katika mechi ya kundi G.

Malkia  ambao ni mabingwa wa Afrika,walipoteza seti ya kwanza kwa alama 17-25, ila wakajizatiti na kunyakua seti ya pili 25-15.

Hata hivyo maji yazidi unga Kenya wakiplemewa seti mbili za mwisho 15-25 na 14-25 na kubanduliwa mashindanoni.

Vidosho wa Kenya wanaonolewa na kocha Geoffrey Omondi watarejea uwanjani Jumatano Adhuhuri dhidi ya Vietnam kwa mchuano wa kufunga ratiba.

Ushindi huo wa Poland uliwafikisha kwa robo fainali wakiongoza kundi hilo kwa pointi 6 sawa na Ujerumani.

Share This Article