Vipusa wa Kenya washinda mechi ya kwanza mashindano ya Dunia ya Voliboli

Kenya waliicharaza Vietnam leo  seti 3-0 za  25-23, 25-22 na 25-18  ukiwa shindi wa tatu katika historia tangu waanze kucheza mashindano ya Dunia.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Voliboli ya wanawake ya Kenya  Malkia Striker, ilisajili ushindi wa kwanza katika mechi ya mwisho ya mashindano ya Dunia yanayoendelea nchini Thailand.

Kenya waliicharaza Vietnam leo  seti 3-0 za  25-23, 25-22 na 25-18  ukiwa shindi wa tatu katika historia tangu waanze kucheza mashindano ya Dunia.

Malkia Strikers walikuwa wamepoteza mechi mbili za awali kundi G seti 3-0 na 3-1 dhidi ya  Ujerumani na Poland mtawalia.

Share This Article