Timu ya taifa ya wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 imefuzu kwa raundi ya tatu ya mechi za kuwania tiketi kushiriki fainali za Kombe la Dunia baada ya kuinyuka Ethiopia mabao 4-0.
Mechio hiyo ya marudio ya raundi ya pili iliyopigwa Jumapili alasiri katika uwanja wa Ulinzi ilishuhudia Elizabeth Mideva, alipachika mabao mawili huku Valerie Nekesa na Fasila Adhiambo wakiongeza moja kila moja.
Kenya imefuzu kwa raundi ya tatu itakapochuana na Tanzania Februari mwaka ujao kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, baada ya mkumbo wa kwanza kumalizikia sare ya bao 1 wiki jana mjini Adis Ababa.