Vipusa wa Kenya waanza CECAFA kwa matao ya juu

Martha Amunyolet alipachika mabao mawili kabla ya Faith Mboya kuongeza la tatu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya taifa ya soka ya wanawake Harambee Starlets, imeanza kampeni ya kuwania kombe la CECAFA, kwa kishindo baada ya kuwagaragaza Burundi mabao 3-0, Jumapili jioni katika uwanja wa Azam Complex, jijini Dares Salaam Tanzania.

Martha Amunyolet alipachika mabao mawili kunako dakika ya 2 na 5, kabla ya Faith Mboya kugongomelea msumari wa mwisho kwenye jeneza la Burundi dakika ya 90.

Kenya chini ya Mwalimu Beldine Odemba, watarejea uwanjani tarehe 17 mwezi huu dhidi ya Uganda kabla ya kumenyana na Sudan Kusini siku mbili baadaye.

Kenya itahitimisha ratiba ya mechi za makundi dhidi ya Tanzania Juni 21.

Share This Article