Baadhi ya viongozi wa eneo la Magharibi mwa nchi wamepuuzilia mbali uvumi na jaribio lolote la kumng’atua spika wa bunge la taifa Moses Wetangula.
Haya yanajiri baada ya uvumi kuenezwa kwamba kuna mpango wa kumbandua Wetangula kutoka kwa wadhifa wa spika wa bunge la taifa.
Wakizungumza katika hafla ya mazishi ya mbunge wa zamani wa eneo la Kimilili Suleiman Murunga, Gavana wa Bungoma Ken Lusaka na mbunge wa sasa wa Kimilili Didimus Barasa walisema jaribio kama hilo litahatarisha ushirikiano kati ya chama cha Ford Kenya na muungano tawala.
Spika Moses Wetangula kwa upande wake aliondolea wakazi wa Magharibi wasiwasi kuhusu kuondolewa kwake madarakani