Idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa wa Kala-azar kwa sasa imefikia 33.
Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni anasema visa vipya 16 vya ugonjwa huo vimerpotiwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Katibu huyo anasema timu kutoka Wizara hiyo imetumwa kwenda kufanya kazi na serikali ya kaunti ya Wajir ili kukabiliana na ugonjwa huo.
Mlipuko wa ugonjwa huo uliripotiwa mwezi Septemba mwaka jana.
Jana Jumatano, Gavana wa kaunti ya Wajir Ahmed Abdullahi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Magavana alisema juhudi zinafanywa kudhibiti ugonjwa huo kwani watu wengi zaidi wanaondoka hospitalini ikilinganishwa na wanaolazwa.
Amehusisha hatua hii na msaada wanaopata kutoka kwa serikali kuu.