Venezuela imekashifu kauli ya Trump kuhusu anga ya nchi hiyo na kuitaja kuwa tishio la ukoloni.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Venezuela ilitoa taarifa kuhusu suala hilo kupitia kwa taarifa rasmi kufuatia wiki kadhaa za mvutano kati ya Venezuela na Marekani.
Rais wa Marekani alitoa tangazo mapema Jumamosi akisema kwamba anga iliyo juu ya Venezuela na inayozunguka Venezuela inapaswa kuchukuliwa kuwa imefungwa kikamilifu.
Katika taarifa ya jana Jumamosi, Wizara ya Mambo ya Nje ya Venezuela ilisema tishio hilo la kikoloni linalenga kuathiri mamlaka ya anga yake, na hivyo kuwa shambulio jingine lisilo la kawaida, lisilo halali na lisilo na msingi dhidi ya watu wa Venezuela.
Trump alitumia mtandao wa Truth Social Jumamosi asubuhi ambapo aliandika, “Kwa Mashirika yote ya Ndege, Marubani, Wauzaji wa Dawa za Kulevya na Wanaouza binadamu, tafadhali zingatieni ANGAYA JUU NA INAYOZUNGUKA VENEZUELA KUWA IMEFUNGWA KABISA.”
Ujumbe huo ulijiri wakati kuna ongezeko la kauli kali kutoka kwa maafisa waandamizi wa Marekani dhidi ya Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na serikali yake.
Utawala wa Trump ukisema unalenga Venezuela kama sehemu ya juhudi za kupambana na usafirishaji wa dawa za kulevya, wataalamu na waangalizi wa haki za binadamu wameonya kuwa inaonekana kuweka msingi wa jaribio la kumwondoa Maduro madarakani kinyume cha sheria.
Marekani imetuma ndege kubeba ndege huko Caribbean na kutekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya meli ilizoshutumu kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kuua watu katika kile wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea kuwa mauaji ya kiholela.
Mapema wiki hii, Trump pia alionya kuwa angeanza kulenga usafirishaji wa dawa za kulevya wa Venezuela kwa njia ya nchi kavu hivi karibuni.
Katika hotuba iliyorushwa kwenye televisheni ya kitaifa Alhamisi, Maduro alisema Watu wa Venezuela hawatatishwa.
Rais wa Venezuela alisema Marekani inaongeza visingizio na uongo ili kuhalalisha uvamizi wa Venezuela, na hayo yalikuwa kabla ya tangazo hili kutolewa na Rais Trump.
Utawala wa Trump umekuwa ukiongeza shinikizo hatua kwa hatua dhidi ya serikali ya Maduro kwa miezi kadhaa.
Mnamo Agosti, Washington ilitoa zawadi ya dola milioni 50 kwa taarifa itakayosaidia kumkamata Maduro, ikidhibiti ujira uliokuwepo awali.
Na mapema wiki hii, Marekani ilitangaza kundi la ukiritimba la Cartel de los Soles linalohusishwa na Maduro, kuwa shirika la kigaidi.
Wavenezuela walianza kutumia jina Cartel de los Soles miaka ya 1990 kumaanisha maafisa waandamizi wa jeshi waliotajirika kupitia biashara ya dawa za kulevya.