Kifo cha Papa Francis siku ya Jumatatu, kilisababishwa na kiharusi na mshtuko wa moyo, haya ni kwa mujibu wa Vatican.
Papa Francis alifariki siku ya Ijumaa katika makazi yake, akiwa na umri wa miaka 88 baada ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki kukumbwa na matatizo kadhaa ya kiafya.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki ambaye sehemu ya pafu moja ilitolewa akiwa kijana, alipambana na matatizo ya kiafya kwa muda mrefu na alikuwa akikabiliwa na magonjwa ya kupumua.
Alilazwa hospitalini kwa wiki tano msimu huu wa baridi baada ya kupata homa ya mapafu.
Papa Francis alizuru Kenya mnamo Novemba mwaka wa 2015 ambapo aliwahimiza Wakenya na mahujaji kutoka kote katika kanda hii, kuishi pamoja kama watoto wa Mwenyezi Mungu, ili kuonyesha mfano halisi wa Mungu anayetunza amani, utangamano na upendo miongoni mwa wanadamu.
Tangu mwaka 2022, mara nyingi alitumia kiti cha magurudumu, kitembezi au fimbo kutokana na majeraha ya goti, na alikuwa kutokana na kuanguka mara nyingi.