Uuzaji wa tiketi kwa makala ya nane ya fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani (CHAN) unaendelea.
Fainali za CHAN zitaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda, na Tanzania kati ya Agosti 2 na 30.
Kenya itaandaa mechi za kundi A ikishirikisha mataifa ya Kenya, Angola, Zambia, DRC, na Morocco.
Mechi ya ufunguzi nchini Kenya itasakatwa Agosti 3 katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani kati ya Harambee Stars na The Leopards ya DRC.
Tiketi kwa mechi za humu nchini zinauzwa kwa shilingi 200 kwa zile za maeneo ya kawaida, 500 kwa tiketi za VIP, na 1,000 kwa eneo la VVIP.
Mechi zote 44 zitarushwa mubasahara kupitia runinga ya taifa KBC Channel 1.