Hali ya utulivu imeripotiwa kurejea mjini Kathmandu, nchini Nepal mapema leo Jumatano, kufuatia maandamano mabaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.
Maandamano hayo ya vijana wa Gen Z yaliyofanyika juzi Jumatatu yalisababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Sharma Oli hiyo jana.
Kiini chake kilikuwa ni kupinga kukithiri kwa ufisadi serikalini.
Nayo ni mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Nepal huku watu 19 wakiripotiwa kuuawa siku ya Jumatatu kwa kupigwa risasi na polisi.
Yamkini watu 25 waliojaribu kuingia barabarani mapema leo katikati ya mji wa Kathmandu walitiwa mbaroni na polisi.
Waandamanaji waliteketeza majengo ya bunge jana Jumanne.