Ushuru unaotozwa kwa kampuni zinazotoa huduma za kamari hapa nchini, umeongezeka hadi shilingi bilioni 13.2 kufikia mwezi Juni, kutoka shilingi bilioni 10.6 mwaka uliopita.
Halmashauri ya Ukusanyaji Ushuru Nchini (KRA), imesema kuwa wakati wa mwaka wa fedha wa 2024/25, ushuru kutoka kwa huduma za kamari ulipita lengo la shilingi bilioni 5.5, baada ya kukusanya shilingi bilioni 5.7.
Kulingana na KRA, hatua hiyo inaashiria ukuaji wa asilimia 22.
Ufanisi huo umeokana na kujumuishwa kwa mifumo ya kampuni za kamari na ile ya KRA, iliyowezesha ufuatiliaji wa malipo ya kamari kwa wakati.
Ukuaji huo unajiri huku taifa hili likiendelea kukabiliwa na changamoto za uchumi.
Kulingana na utafiti wa kiuchumi wa mwaka 2025, uchumi wa taifa hili ulikua kwa asilimia 4.7 mwka 2024, kutoka asilimia 5.7 mwaka 2023.