Usalama waimarishwa Homa Bay kabla ya Siku Kuu ya Madaraka

Tom Mathinji
1 Min Read
Mrakibu wa eneo la Nyanza Flora Mworoa.. Picha/ Jackson Mnyamwezi.

Kaunti ya Homa Bay imejiandaa vilivyo kuwa mwenyeji wa sherehe za mwaka huu za Siku Kuu ya Madaraka, zitakazoandaliwa katika uwanja wa Raila Odinga, haya yamethibitishwa na Mrakibu wa eneo la Nyanza Flora Mworoa.

“Tumejitayarisha vilivyo kuwa mwenyeji wa sherehe za Siku Kuu ya Madaraka ya mwaka huu katika uwanja wa Raila Odinga,” alisema Mworoa.

Aidha, kama sehemu ya kuimarisha muundo msingi katika eneo hilo, Mrakibu huyo alisema kuwa Ikulu ndogo ya kisasa imejengwa katika eneo hilo, kuwashughulikia wageni wa ngazi za juu watakaohudhuria sherehe hiyo.

Alidokeza kuwa barabara mjini Homa Bay zimefanyiwa ukarabati, kuimarisha shughuli za usafiri.

 “Sasa tuna barabara ya safu mbili kutoka Mbita hadi katika uwanja wa Raila Odinga, kuhakikisha wananchi hawatatiziki wanaposafiri kuingia Homa Bay,” alisema Mworoa.

Share This Article