Usaili wa mwenyekiti mpya wa IPOA kuandaliwa Oktoba 22 na 23

Dismas Otuke
1 Min Read
Anne Makori - Mwenyekiti wa IPOA anayeondoka

Mahojiano ya kumtafuta mwenyekiti mpya wa Mamlaka Huru ya Kuangazia Utenda Kazi wa Maafisa wa Polisi, IPOA yataandaaliwa kati ya Oktoba 22 na 23.

Wadhifa huo kwa sasa unashikiliwa na Anne Makori anayeondoka.

Watu wanane wamealikwa kwa mahojiano hayo huku wengine 37 wakiitwa kwa mahojiano ya kuwa mwanachama wa mamlaka hiyo.

Wanane waliopasi mchujo wa mwenyekiti wa IPOA ni aliyekuwa kamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC Thomas Letangule, Annah Konuche, Patrick Blasius Owiny na Mercy Wambui Kamau watakaosailiwa Oktoba 22.

Watakaohojiwa siku ya pili ni pamoja na aliyekuwa mwenyekiti wa IEBC Ahmed Issack Hassan, Wayong’o Cyril Simiyu, Juliet Wanjiku Muremi na Richard Barno.

Mahojiano ya wanaokusudia kuwa wanachama wa IPOA yatafanyika kuanzia tarehe Oktoba 24 hadi 30, kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

TAGGED:
Share This Article