Urithi: Viongozi wa Kiislamu wapinga uamuzi wa Mahakama ya Juu

Martin Mwanje
1 Min Read

Viongozi wa Kiislamu nchini Kenya wamepinga vikali uamuzi wa hivi majuzi wa Mahakama ya Juu unaoruhusu watoto waliopatikana nje ya ndoa kurithi mali za baba zao Waislamu.

Wakizungumza mjini Kakamega, mwenyekiti wa NAMLEF Kanda ya Magharibi Sheikh Abu Muhsin Kassim, Suleiman Anami, na Mwenyekiti wa SUPKEM kaunti ya Kakamega Sheban Wafula wamesema uamuzi huo unatishia uhuru wa kidini na uhuru wa taasisi za kisheria za Kiislamu.

Mgogoro huu ulitokana na kesi iliyowasilishwa na Fatuma Athman Abud Faraj, aliyekuwa akitaka kuwazuia watoto waliopatikana nje ya ndoa yao kurithi mali ya marehemu mumewe, Salim Juma Hakeem Kitendo.

Katika kikao hicho, viongozi hao pia walipinga ujenzi wa kanisa ndani ya Ikulu ya Nairobi, wakionya kuwa hatua hiyo inaweza kuchochea mgawanyiko wa kidini.

Share This Article