Upinzani Tanzania wahimizwa kuzingatia sheria

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa wito kwa vyama vya kisiasa nchini humo kuzingatia sheria na kuhakikisha kuwa amani ya taifa inadumishwa kila wakati.

Matamshi ya Rais huyo yanajiri siku moja baada ya wafuashi wa Chama cha Demokrasia na Mapinduzi(CHADEMA), kukabiliana na maafisa wa polisi nje ya Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, wakitaka kuhudhuria kesi inayomkabili kiongozi wa chama hicho Tundu Lissu.

Kwa mujibu wa CHADEMA, vurugu hizo zilisababisha kukamatwa kwa viongozi waandamizi wa chama hicho akiwemo Makamu Mwenyekiti John Heche na Katibu Mkuu John Mrema, huku wakidai kuwa mtu mmoja alipoteza maisha na wengine kadhaa walijeruhiwa.

Chama hicho kilionyesha baadhi ya majeruhi mbele ya wanahabari pamoja na wawakilishi wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International, na Chama cha Mawakili kutoka Kenya.

Share This Article