Muungano wa upinzani Azimio one Kenya, umetangaza kurejele maandamano ya kupinga gharama ya maisha tarehe 12 mwezi baada ya kufanya maandamano ya siku ya sabababa.
Muungano huo chini ya ungozi wa kinara wa chama cha ODM Ralila Odinga pia umetishia kuishtaki serikali kwa kushindwa kuwapqa ulinzi na kushambuliwa kwa vitoa machozi wakati wa maanadamano ya Julai 7.
kulingana na kiranja wa walio wacheche bungeni Opiyo Wandayi maandamano ya siku ya Ijumaa yalikuwa yakuwaandaa wafuasi wao kote nchini kujitokeza na kulalamikia gharama ya juu ya maisha na mswada wa fedha wa mwaka 2023.
Maafisa wa usalama walikabiliana na waandamaji hao katika kaunti mbali siku ya Jumatano.