Upasuaji wa maiti ya MCA wa Kariobangi, Joel Munuve, kufanyika leo

Idara ya DCI pia imeingilia kati uchunguzi huo na kulazimu upasuaji wa maiti ya marehemu uliokuwa ufanyike jana kuaahirishwa hadi leo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Upasuaji wa maiti ya mwakilishi wadi wa Kariobangi Kaskazini, Joel Munuve, utafanyika leo katika juhudi za kutaka kubaini kiini cha kifo chake.

Familia ya marehemu mwanasiasa huyo, kupitia kwa wakili , Dunston Omari, ilitaka upasuaji kufanyika ili kuondoa uvumi unaozagaa kuhusiana na chanzo cha kifo chake.

Idara ya DCI pia imeingilia kati uchunguzi huo na kulazimu upasuaji wa maiti ya marehemu uliokuwa ufanyike jana kuaahirishwa hadi leo.

Mwakilishi wadi huyo kwa wakati mmoja alikuwa ametishia kuwasilisha mswada wa kumtimua Gavana Johnstone Sakaja.

Share This Article