Spika Moses Wetang’ula anaongoza uongozi wa Bunge la Taifa kwenye mkutano wa siku tatu ulioanza leo Alhamisi mjini Mombasa.
Mkutano huo ni wa tatu kuwahi kuandaliwa tangu kuasisiwa kwa bunge la 13.
Unawaleta pamoja Makamishna wa Tume ya Huduma za Bunge, PSC, wanachama wa jopo la maspika, wenyeviti wa kamati mbalimbali na manaibu wao miongoni mwa taasisi zingine.
Lengo ni kutafuta mbinu za kuboresha utenda kazi wa bunge hilo kwa manufaa ya Wakenya.

Mkutano huo unakuja wakati madai ya kukithiri kwa ufisadi bungeni yamezagaa kotekote.
Bunge la Taifa limeenda kwa likizo fupi na litarejelea vikao vyake Septemba 23.