Umaarufu wa uchumi wa China nchini Kenya na duniani waendelea kukua huku wa Marekani ukipungua

Eric Biegon
2 Min Read

Utafiti wa mpya uliofanyika hivi karibuni unaonesha kuwa China imejijengea sifa kubwa miongoni mwa Wakenya, kuwa ni mshirika anayepewa kipaumbele kiuchumi duniani katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, huku ushawishi wa Marekani ukiendelea kupungua.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kituo cha Utafiti cha Pew, kilicho chini ya taasisi ya washauri bingwa mjini Washington, DC, sehemu ya Wakenya wanaotaka serikali iweke kipaumbele katika uhusiano wa kiuchumi na China imeongezeka kwa asilimia 10 kutoka mwaka 2019 hadi asilimia 48 mwaka 2025, na kuwa sawa na Marekani.

Hii inaonesha kuongezeka kwa ushawishi wa China nchini Kenya, uchumi wa pili kwa ukubwa duniani. Alama za Marekani za mshirika wa kiuchumi anayependelewa zaidi zimepungua kutoka asilimia 52 hadi 48 katika kipindi cha kabla ya janga la COVID-19.

Kituo cha Pew kimesema kwenye utafiti huo uliofanyika kuanzia Januari 8 hadi Aprili 26, 2025, umeonyesha kuwa katika miongo moiwili iliyopita, China imekuwa na ushawishi wa kiuchumi kwa Kenya kupitia miradi yake ya maendeleo ya miundombinu kupitia mpango wa Ukanda Mmoja, Njia moja (BRI) – uliozinduliwa mwaka wa 2023.

Kenya imekuwa mmoja wa wapokeaji wakubwa wa uwekezaji kupitia mpango wa BRI, ikiwa ni pamoja na reli ya SGR inayotoka Mombasa hadi Nairobi, barabara kuu ya Nairobi yenye urefu wa kilomita 27, barabara kuu ya Thika yenye urefu wa kilomita 50, na miradi mingine.

Kwenye nchi tisa zenye kipato cha kati ziliyofanyiwa utafiti, wastani wa asilimia 58 wanasema uwekezaji kutoka China ni mzuri kwa sababu unaleta nafasi za ajira.

Share This Article