Ulinzi wa Kindiki waimarishwa maradufu

Dismas Otuke
1 Min Read

Ulinzi wa Naibu Rais Mteule Abraham Kithure Kindiki uliimarishwa jana jioni maradufu, punde baada ya mahakama huu kuruhusu kuapishwa kwake .

Imebainika kuwa zaidi ya maafia wa polisi 50 walipelekwa nyumbani kwake Tharaka na pia jijini Nairobi, ili kumwongezea ulinzi anaostahiki Naibu Rais.

Pia usalama umeimarishwa katikati ya jiji la Nairobi kuanzia mapema Ijumaa,huku kila anayeingia katika ukumbi wa KICC akikaguliwa mara kadhaa.

Kindiki ataapishwa kutwaa mikoba ya Unaibu Rais kutoka kwa Rigathi Gachagua, aliyetimuliwa na Wabunge 232 kabla ya Maseneta kuidhinisha kufurushwa kwake.

Gachagua alielekea mahakamani kutaka uamuzi huo ubatilishwe na kuzuia uapisho wa Kindiki ,ila hatimaye mahakama kuu ikaidhinisha kuapishwa kwa Kindiki.

Share This Article