Ukraine na Urusi zakubaliana kubadilishana wafungwa wa kivita

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa wa Ukraine na Urusi washiriki mazungumzo ya ana kwa ana.

Ukraine na Urusi zimekubaliana kubadilishana wafungwa wa kivita, hayo ni kwa mujibu wa Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Rustem Umerov.

Akizungumza na wanahabari baada ya mkutano kati ya Ukraine na Urusi, waziri huyo alisema kuwa kupitia makubaliano hayo, kila nchi itawaachilia wafungwa 1,000.

“Tumejadili swala la kumaliza mapigano. Na suala la kubadilishana wafungwa. Matokeo yake ni kubadilishana watu 1,000 kwa 1,000.

Hata hivyo, waziri huyo alidokeza kuwa siku yakutekeleza makubaliano hayo, bado haijatangazwa wazi.

“Tarehe ya kutekeleza mpango huo imewekwa, lakini haijawekwa wazi” alisema waziri huyo.

Umerov pia anasema uwezekano wa kufanyika kwa mkutano kati ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin ulijadiliwa na kwamba tangazo kuhusu duru mpya ya mazungumzo litatangazwa hivi karibuni.

“Njia zote” za kusitisha mapigano pia zilijadiliwa, aliongeza Umerov.

TAGGED:
Share This Article