Ukarabati wa uwanja wa Raila Odinga kukamilika mwezi Mei

Tom Mathinji
1 Min Read
Uwanja wa Raila Odinga.

Kazi ya upanuzi na ukarabati wa uwanja wa Raila Odinga inatarajiwa kukamilika na kukabidhiwa serikali ya taifa kufikia Mei,15 2025 kwa matayarisho ya sherehe zijazo za siku kuu ya Madaraka.

Akizungumza alipofanya ziara ya ukaguzi katika uwanja huo, Katibu wa usalama wa kitaifa Dkt. Raymond Omollo,  alithibitisha hayo akisema kazi hiyo ya ukarabati inakaribia kukamilika.

“Ziara yetu ililenga kukadiria matayarisho kabla ya sherehe ya Madaraka, tukiangazia sana miundombinu, usafiri na usalama,’ alisema Dkt. Omollo.

Akiwa ameandamana na Gavana wa Homa Bay Gladys Wanga, Dkt. Omollo aliongeza kwamba kazi ya ujenzi wa ikulu ndogo ya Rais katika sehemu hiyo pia inakaribia kukamilika,huku ikulu hiyo ndogo ikitarajiwa kukabidhiwa serikali kati kati mwa mwezi ujao.

Ikulu hiyo pia itatumika kwa dhifa ya chakula cha mchana kwa wageni mashuhuri watakaohudhuria sherehe za Madaraka Day.

Uwanja wa michezo wa Raila Odinga, utatumika kwa maadhimisho rasmi ya siku kuu ya Madaraka, Juni 1,2025.

Kazi ya upanuzi na ukarabati wa uwanja huo ilizinduliwa baada ya rais William Ruto kutangaza kwamba uwanja huo utakuwa ukitumika kwa sherehe rasmi za kitaifa na kuagiza hazina kuu kutenga fedha za upanuzi wake.

Share This Article