‘Kawia ufike’e’ ni msemo wa Kiswahili ambao kwa sasa una mashiko kwa wakazi wa Laikipia walioathiriwa na mkasa wa moto mwaka 2021, baadaa ya Serikali ya Uingereza kuwalipa fidia kutokana na na mkasa wa moto uliosababishwa na wanajeshi wake wa kundi la 3rd Battalion wakiwa mazoezi.
Uingereza imekubali kulipa fidia ya dola za Marekani milioni 4,sawa na shilingi milioni 520 za Kenya, kwa wakazi wa Laikipia wapatao 7,000, ambao walipoteza mali yao kutokana na mkasa wa moto uliotokea mbugani uliosababishwa na mazoezi ya wanajeshi hao wa Uingereza.
Moto huo ulitokea karibu na milima ya Lolldaiga, wakati wanajeshi hao wakifanya mazoezi ya kukabiliana na vilipuzi.
Wakili wa waathiriwa alithibutisha pesa hizo zimelipwa kwa waathiriwa wote.