Uhuru miongoni mwa viongozi waliotambuliwa na WHO

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta.

Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta ni miongoni mwa viongozi waliotambliwa rasmi na Shirika la Afya Duniani (WHO) kutokana na mchango wake katika kufanikisha utekelezaji wa mkataba wa kukabiliana na majanga wa shirika hilo.

Wakati wa hafla maalum iliyoandaliwa Julai 10, 2025 katika Makao Makuu ya WHO jijini Geneva nchini Uswizi, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus alipongeza  mchakato wa kisiasa uliosababisha ufanisi wa mkataba huo.

“Utekelezwaji wa mkataba wa majanga na Baraza la Afya Duniani, ulikuwa hatua ya kihistoria katika sekta ya afya duniani. Lakini hatungeafikia hayo bila uungwaji mkono wa kisiasa kutoka ngazi za juu,”alisema Ghebreyesus.

Uhuru anajiunga na viongozi wa sasa na wa zamani waliotambuliwa kutokana na mwongozo na kujitolea kwao kuhakikisha mkataba huo unaafikiwa, unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia, kujiandaa na kukabiliana na majanga.

Kenya ilitambuliwa pamoja na nchi zingine 24 zikiwemo Ufaransa, Ujerumani, Indonesia, Rwanda, Senegal, Uingereza na Jamhuri ya Korea.

Zingine ni Albania, Costa Rica, Croatia, Fiji, Ufaransa, Ugiriki, Italia, Uholanzi na Ureno miongoni mwa zingine.

Share This Article