Ugonjwa wa Chikunyunga wazuka Mombasa

Tom Mathinji
1 Min Read
Ugonjwa wa Chikungunya wazuka kaunti ya Mombasa.

Ugonjwa wa Chikungunya umeripotiwa kuzuka katika kaunti ya Mombasa.

Ugonjwa huo uligunduliwa baada ya sampuli 45 kufanyiwa uchunguzi na Taasisi ya Utafiti wa Matibabu (KEMRI), ambapo sampuli 25 zilipatikana kuwa na ugonjwa huo, huku sampuli moja ikipatikana kuwa na homa ya Dengue.

Ugonjwa huo ambao huambukizwa binadamu kutoka kwa wadudu kama vile mbu, husababisha maumivu kwenye misuli na viungo vingine vya mwili.

Kulingana na watafiti, mabadaliko ya Tabia Nchi, ambayo yamesababisha kuongezeka kwa hali ya joto na mvua kubwa, kunatoa fursa kwa mbu walio na ugonjwa huo kuenea zaidi na kuwaambukiza binadamu ugonjwa huo.

Chikungunya ni neo la Kimakonde nchini Tanzania, linalomaanisha kuinama kutokana na maumivu ya ugonjwa huo.

Share This Article