Uganda, Morocco na Mali zafuzu raundi ya 16 bora Kombe la Dunia kwa miaka 17

Dismas Otuke
1 Min Read

Uganda, Morocco na Mali zimefuzu kwa awamu ya timu 16 bora, katika fainali za Kombe la Dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 17 zinazoendelea nchini Qatar.

Morocco ilifuzu Ijumaa baada ya kuwalemea Marekani mabao 4-2 kupitia penati kufuatia sare ya 1-1.

Mali pia ilijakatia tiketi Ijumaa baada ya kuwashinda Zambia mabao 3-1, huku Uganda ikiwatema nje Senegal goli moja kwa bila siku ya Jumamosi.

Mali watamenyana na Morocco kuwania tiketi ya kucheza robo fainali wakati Uganda ikisubiri mshindi kati ya Burkina Faso na Ujerumani.

Share This Article