Uganda kuwasilisha bajeti ya shilingi trilioni 40.7

Waziri wa fedha wa Uganda Henry Musasizi ,anatarajiwa kusoma bungeni bajeti ya shilingi trilioni 40.7, sawia na shilingi trilioni 1.4 za Kenya.

Dismas Otuke
1 Min Read

Leo ni siku ya kusomwa kwa bajeti ya makadirio ya matumizi ya fedha ya mwaka 2025 na 2026 kwa mataifa mengi ya Afrika Mashariki.

Waziri wa fedha wa Uganda Henry Musasizi ,anatarajiwa kusoma bungeni bajeti ya shilingi trilioni 40.7, sawia na shilingi trilioni 1.4, za Kenya.

Wizara ya ulinzi imetengewa shilingi trilioni 3.737, ili kuimarisha ulinzi ,shilingi trilioni 5.69, zikitengewa ukarabati wa miundo mbinu ya barabara, huku Wizara ya kawi ikitengewa shilingi trilioni 1.58.

Sekta ya afya itapokea mgao wa shilingi trilioni 1.39,elimu kupata shilingi bilioni 497.1, na bilioni 611.5, katika sekta ya kilimo.

Aidha, serikali ya Uganda inakadiria ongezeko la pato lake kutoka kiwango shilingi trilioni 31.9, katika mwaka wa kifedha unaokamilika hadi shilingi trilioni 33.6.

Share This Article