Uganda Cranes imewashinda mabingwa watetezi wa CHAN Senegal kwa mabao 2-1, katika mechi ya pili baina ya mataifa matatu ya CECAFA iliyosakatwa leo mjini Arusha, Tanzania.
Arnold Odong na Patrick Kakande, walipacika magoli ya Uganda dakika za 64 na 67 mtawalia huku Simba wa Teranga wakifunga bao pekee dakika ya 87 kupitia kwa Moctar Koite.
Cranes walikuwa wameshindwa bao moja kwa bila na Tanzania siku ya Jumatatu.
Timu hizo zinatumia mashindano hayo yatakayokamilika Julai 27 kujiandaa kwa makala ya nane ya kipute cha CHAN.
Senegal wamo kundi D pamoja na Nigeria, Congo, na Sudan, wakati Uganda wakijumuishwa kundini C pamoja na Algeria, South Africa, Guinea, na Niger.