Katika harakati za kuinua kiwango cha elimu kwa jamii maskini, shule ya msingi na ya upili ya Vota itapata majengo mapya yatakayogharimu shilingi milioni 51 kutoka kwa wakfu wa Mpesa Foundation.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ufadhili huo huko VOTA, Machakos, Patricia Ithau, afisa wa wakfu huo ameeleza kwamba shule hizo mbili zitapata majengo hayo mapya ili kuinua hadhi yake na kusaidia wanafunzi maskini kupata elimu katika mazingira safi.
Aliongeza kuwa kufikia sasa, zaidi ya shule 350 nchini zimefaidi kutokana mpango huo na kupata majengo mapya ya kisasa tangu kuanzishwa kwa mpango huo.
Katika ujenzi huo, shule hizo mbili zitapata madarasa mapya, maktaba ya kisasa na uwanja wa michezo kwa wanafunzi.