UDA kuandaa chaguzi za mashinani mwezi ujao

Dismas Otuke
1 Min Read

Chama cha United Democratic Alliance (UDA), kimetangaza kuandaa chaguzi za mashinani katika kaunti 22 nchini kati ya tarehe 11 na 12 mwezi ujao.

Kaunti zitakazoandaa chaguzi hizo ni pamoja na Bungoma, Garissa, Isiolo, Kajiado, Kilifi, Kisii, Kisumu, Kitui, Kwale, Lamu, Machakos, Makueni, Wajir, na Mandera.

Kaunti zingine ni Marsabit, Migori, Mombasa, Nyamira, Siaya, Taita Taveta, Tana River, na Turkana.

Wawaniaji 113,800 tayari wamejisajili kushiriki chaguzi hizo huku usajili ukifungwa Ijumaa, Machi 21.

Kulingana na Mwenyekiti wa UDA Cecily Mbarire, tayari wamekamilisha uchaguzi huo katika kaunti 5 na pia wamenunua vifaa vya kielektroniki 10,000, kujiandaa kwa zoezi hilo la mwezi ujao.

Mbarire, ambaye pia ni Gavana wa Embu, amesema vifaa hivyo vitasaidia kuandaliwa kwa uchaguzi huo kwa njia ya wazi na huru.

Share This Article